Gari aina ya Costa, lenye namba za usajili T374AVR, likiwa limepinduka baada ya kugongwa na basi la El Saedy juzi, asubuhi na kujeruhi abiria waliokuwemo kwenye basi hilo. Katika ajali hiyo, iliyotokea Imezu Wilaya ya Mbeya Vijijini zaidi ya watu 40, walijeruhiwa.
Wananchi wakiliangalia gari aina ya Costa lenye namba T 374 AVR, lililopata ajali baada ya kugongwa na basi la Kampuni ya El Saedy juzi, asubuhi. Ajali hiyo ililiacha basi hili dogo, lililokuwa na maandishi ya Survival likiwa limeharibika vibaya.
No comments:
Post a Comment