Waasi wa Tuareg nchini Mali wameutwaa mji wa Kidal kaskazini mwa Mali,wiki moja tu baada ya wanajeshi kuipindua serikali, wakisema kuwa jeshi linahitaji silaha za kupambana na waasi hao.
Msemaji wa waasi aliambia BBC kuwa wamethibiti mji huo, tamko lililothibitishwa na raia wa eneo hilolo
Kiongozi wa waasi waliopindua serikali, Amadou Sanogo ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia jeshi kupambana na waasi hao.
Shirika la nchi za kanda ya Magharibi mwa Afrika, ECOWAS, limelaani kitendo cha wanajeshi, huku nchi hizo zikitishia kuiwekea vikwazo Mali.
Viongozi wa nchi za magharibi mwa Afrika wamewapa wanajeshi waliopindua serikali ya Mali makataa ya saa 72 kuondoka madarakani au waadhibiwe kwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.
Viongozi hao wametangaza kuwa watafunga mipaka yote ya Mali na kufunga akaunti ya nchi hiyo.
Hii ni baada ujumbe mzito wa viongozi wa ECOWAS kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bamako kutokana na maandamano makubwa ya kuunga mkono mapinduzi hayo.
Viongaoi wa ECOWAS,walikutana Ivory Coast, baada ya mpango wao kwenda kwa mazungumzo na viongozi wa wanjeshi waasi , Mali kutibuka.
No comments:
Post a Comment