Wanajeshi walionyakua madaraka Mali wamesema hawana azma ya kubaki madarakani na wataondoka papo msukosuko wa ndani ya nchi umepatiwa ufumbuzi.
Mwanajeshi mmoja kati ya hao waasi, Kanali Moussa Coulibaly, alisema baada ya kufanya mazungumzo nchi ya jirani ya Burkina Faso, kwamba hawana azma ya kunyakua madaraka.
Mapigano zaidi yametokea kaskazini mwa Mali ambako wapiganaji wa kabila la Tuareg wanaendelea kusonga mbele, na wameingia kwenye mji muhimu wa Gao kushambulia majeshi ya serikali.
Mwandishi wa BBC wa Afrika Magharibi anasema jumuia ya eneo hilo, Ecowas, imeweka wanajeshi 2,000 katika hali ya matayarisho, iwapo itahitajika kuingia kwa nguvu nchini Mali.
No comments:
Post a Comment