TANGAZO


Friday, March 23, 2012

Uvunjaji nyumba zilizokuwa za Shirika la Reli na Mamlaka ya Bandaria Tanzania

Picha
Vijana wakiezua moja ya nyumba zilizokuwa za Shirika la Reli na Mamlaka ya Bandari, maeneo ya Shule ya Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuvunjwa kutokana na amri ya Mahakama Kuu, kwa ajili ya kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi ya jiji. (Picha zote na Kassim Mbarouk) 


Tingatinga la Kampuni ya Jandu, likiwa kazini kuvunja nyumba hizo chini ya usimamizi wa Kampuni ya mnda ya Yono.


Maofisa wa Jeshi la Polisi wakisimamia utekelezaji wa zoezi hilo, lililokuwa likilalamkiwa na wakazi wa nyumba hizo.


Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Yono, wakiwa kwenye uangalizi wa zoezi hilo, huku matingatinga yakiendelea na uvunjaji wa kota hizo.



Baadhi ya Askari Polisi, wakisimamia utekelezaji wa zoezi hilo.


Baadhi ya wakazi wa kota hizo, wakiwa wametoka kwenye nyumba hizo na kuweka mizigo yao nje nyumba hizo ili kupisha tingatinga kuvunja nyumba hizo.



Vijana wakingoa moja ya vyuma vya umeme kwenye moja ya nyumba zilizo.



Kijana akiwa amebeba kiroba, ambacho hakikuweza kufahamika alichokuwa amekibeba ndani yake.


Binti, mmoja wa wakazi wa nyumba hizo, akitoa begi lake, ili kupisha tingatinga liendelee na kazi yake ya kuvunja nyumba hizo.



Akinamama waliokuwa wakiishi kwenye nyumba hizo, wakitoa magodoro na vitu vingine vilivyokuwa ambavyo vilikuwa havijatolewa kwenye nyumba hizo.


Mmoja wa wakazi wa nyumba hiyo, akitoa godoro, kwa ajili ya kupisha uvunjaji wa numba hizo.



Akina dada wakitoa kochi kwenye moja ya nyumba hizo, kwa ajili ya kupisha zoezi hilo.



Tingatinga likivunja mmoja ya nyumba iliyokuwa kando kando ya mtaa wa Lindi, zilipo nyumba hizo'



Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Umeme la Tanesco, wakipita kwenye mitaa zilipo nyumba hizo, ili kutoa huduma ya kuondoa mita pamoja na nyaya za umeme zilizokuwa kwenye nyumba hizo.


Mmoja wa akinamama waliokuwa wakiishi kwenye moja ya nyumba hizo, akiondoa mbao zilizokuwa zikiondolewa kwenye mapaa ya nyumba hizo.


Wananchi wakiangalia zoezi hilo, lilivyokuwa likitekelezwa na kampuni ya Yono Auction Mart ya jijini Dar es Salaam.


Moja ya mtaa maarufu jijini Dar es Salaam, mtaa wa Msimbazi, ukiwa hauna watu kutokana kuzuiwa kupita kwenye eneo hilo.



Baadhi ya wananchi wakiwa wamefunga mtaa wa Msimbazi ili kujionea wenyewe zoezi hilo lilivyokuwa likiendelea.

Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Yono, akiwazuiya watu wasiingie kwenye eneo la zoezi hilo, ili kuepuka upoteaji wa vifaa pamoja na vitu mbalimbali vilivyokuwa havija tolewa kwenye nyuma hizo wakati wa zoezi hilo.



Tingatinga likiwa kazini, kubomoa moja ya nyumba hizo kwa ajili ya unjenzi wa kituo cha mabasi ya jiji.



Kijana akiwa amejificha ili asipigwe picha, akiwa chini ya setlight  disha ya mmoja wa waliokuwa wakazi wa nyumba hizo.


Baadhi ya nyumba zilizokuwa zinataka kubomolewa, zikiwa zimeshatolewa milango yake kwa ajili ya kupisha Tingatinga kuvunja nyumba hizo.

No comments:

Post a Comment