Tume ya uchaguzi ya Kenya imetangaza rasmi kuwa uchaguzi mkuu utafanywa tarehe 4 mwezi Machi mwaka ujao, baada ya malumbano ya majuma kadha kati ya wanasiasa wanaopingana.
Hata hivo serikali ya mseto ya Kenya ikisambaratika, huenda ikabidi kufanya uchaguzi mapema.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Isaack Hassan, alisema tume ilibidi kutoa kauli, baada ya Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu, Raila Odinga, kushindwa kufikia uamuzi wa pamoja juu ya tarehe.
Alisema nchi inahitaji kujua tarehe.
Uchaguzi huo utakuwa wa mwanzo tangu ule wa mwaka 2007 kuzusha fujo ambapo watu zaidi ya 1000 walikufa.
No comments:
Post a Comment