Mechi kati ya Kombe la FA kati ya Tottenham na Bolton Wanderers ilisimamishwa ghafula baada ya mchezaji wa Bolton, Fabrice Muamba kuzimia ghafula, na kushindwa kuvuta pumzi.
Madaktari walijaribu kwa dakika 10 kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aweze kupumua, na hilo liliposhindikana, ilimlazimu mwamuzi Howard Webb kusimamisha mchezo.Mwandishi wa BBC Radio 5, Ian Dennis, alielezea kwamba mchezaji huyo kiungo cha kati inaelekea alikuwa katika hali ya taabani.
Mchezo ulikuwa ni sare ya 1-1 wakati mechi iliposimamishwa katika dakika ya 41.
Muamba alizaliwa tarehe 6 Aprili mwaka 1988 mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na aliimarika kisoka katika chuo cha vijana wadogo cha Arsenal, na akiiwakilisha England katika mechi mbalimbali, tangu zile za vijana wa miaka 16, hadi zile za wale wa miaka 21.
Alijiunga na Birmingham mwaka 2007, na kuhamia Bolton mwaka uliofuata.
Muamba alicheza katika mechi za Ulaya mwaka 2011, za vijana wa chini ya umri wa miaka 21, akiichezea England katika mashindano yaliyofanyika nchini Denmark.
Tangu kufikishwa hospitali, hakuna habari zaidi zilizotolewa kuhusiana na hali yake ya afya hadi sasa.
No comments:
Post a Comment