TANGAZO


Saturday, March 3, 2012

SIMBA yazindua Television Dar es Salaam



Mchezaji wa Simba, Felix Sunzu, akimkabidhi jezi yake, mgeni rasmi katika uzinduzi wa Televisheni ya klabu ya Simba, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa (wa pili kushoto), aliyopewa katika hafla ya uzinduzi  wa TV hiyo, ambayo itaanza kwa kurusha vipindi vya mambo mbalimbali yanayohusu klabu hiyo na baadaye kuanza kurusha vipindi vyake masaa 24.  Hafla hiyo, ilifanyika jana usiku, Quality Center, jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwanachama timu hiyo, Profesa Juma Kapuya, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange Kaburu na Mwenyekiti wa klabu Ismail Aden Rage. (Picha na Mpiga picha wetu)


Mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba, Zamoyoni Mogella,  akizungumza katika uzinduzi huo, ambapo aliwaasa wachezaji wa timu hiyo, kuonyesha uwezo wao wote hasa katika mchezo wa kesho kati ya Simba na Kiyovu ya Rwanda. Kulia ni Msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kwamwanga.


Mgeni rasmi, Naibu Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa, akimlisha keki, Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage wakati wa hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Makamu wa pili wa TFF, Ramadhan Nassib, Profesa Juma Kapuya na kulia ni Mzee Kinesi.


Mgeni rasmi Naibu, Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa akikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa televisheni hiyo. Kutoka kushoto ni Makamu wa pili wa TFF, Ramadhan Nassib, Profesa Juma Kapuya, Mzee Kinesi (kulia) na Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro, George Kavishe.


Mgeni rasmi Naibu Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe cha kompyuta tayari kwa kuwasha kipindi cha Televisheni kinachoonyesha matukio mbalimbali ya klabu ya Simba. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu, Mwanachama wa Simba,  Profesa Juma Kapuya na kutoka kushoto ni Msemaji hiyo, Ezekiel Kamwanga  na Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage.


Wanaofungua shampeni, kutoka kulia ni Charles Hamka, Said Tuli na Swedi Mkwabi.


Shabiki mkubwa wa Yanga, Motisha naye, alihudhuria katika sherehe hiyo, hapa akitambulishwa huku mwalimu wa makipa wa Simba, James Kisaka, akimuwekea jezi ya Simba.


Mchezaji wa timu ya Simba, Said Nasoro Cholo, akitambulishwa katika hafla hiyo.


Wazee wa Friends of Simba, wakibadilishana mawazo kutoka kulia ni Evance Aveva, Nick Magarinza, Juma Pinto, Salim Try Again, na Redemptus Masanja wa NBC.


Mashabiki na wadau mbalimbali wa Simba wakiwa katika hafla hiyo.


Waandishi wa habari kutoka kulia, Dina Ismail, Jesca Charles, na Asha Kigundula wakiwa katika hafla hiyo.


Kutoka kulia ni Jerry, Bawazir, Musley na Hassan Hasanoo wa Friends of Simba.


Wachezaji wa timu ya Simba wakiwa katika hafla hiyo.


Baadhi ya wachezaji wa timu ya Simba, wakiwa katika hafla hiyo. 

No comments:

Post a Comment