TANGAZO


Sunday, March 18, 2012

Serikali yapongeza Mejimenti ya chama cha wakulima Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa, akilijaribu moja ya matrekta 16 yaliyokabidhiwa kwa vyama vya msingi vya ushirika ikiwa ni mkopo toka benki ya CRDB, tawi la Tabora ambapo mkopo huo umedhamiwa na WETU cha kiuu cha ushirika wa wakulima wa Taumba kanda ya magharibi.

Na Hastin Liumba,Tabora
SERIKALI mkoa wa Tabora,imepongeza menejimenti ya chama cha wakulima wa tumbaku kanda ya magharibi,(WETCU),meneja wa bebki ya CRDB na vyamavya ushirika,kwa kutambua umuhimu wa matumizi ya zana kisasa za kilimo.
Hayo yalisemwa na mkuu wa mkoa wa Tabora,Fatma Mwassa,wakati alipokuwa akikabidhi matreketa 16 waliyokopeshwa vyama vya msingi ya vyaushirika,katika hafla iliyofanyika ofisi za chama cha ushrika cha wakulima wa tumbaku kanda ya magharibi (WETCU).
Mwassa alisema ni ukweli usiopingika kuwa hatua hiyo itasaidia sana katika katika kukuza kilimo chetu hasa katika utelezaji wa mapinduzi ya kijani na kauli mbiu ya kilimo kwanza kutelezwa kwa usahihi zaidi.
Aidha aliwataka wakulima ama vyama vya msingi vilivyokopeshwa kuhakikisha vinarejesha kwa wakati mikopo hiyo, ikiwemo matumizi ya zana hizo kutumika kama ilivyokusudiwa
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka viongozi wa vyama vya msingi kuachadhuluma kwa wakulima hasa wa tumbaku na kamwe hatakubali hali hiyoinaendelea kipindi chake akiwa mkuu wa mkoa wa Tabora.
Akizungumzia kilimo cha tumbaku Mwassa alisema katika kipindi cha toka mwaka 2008 hadi 2011 jumla ya zaidi ya dola sh milioni 252.6
zilipatikana kutokana na mauzo ya tumba tani 132753949.
Alisema hizo ni pesa nyingi lakini kasi ya maendeleo hailingani na mapato halisi yanayopatikana nashauri pia juhudi  ziendelee kufanyika ili mapato haya yaboreshe maisha ya kaya moja moja,makazi bora chakula na lishe bora,utunzaji mazingira ,afya na miundombinu.
”Natoa wito kwa halmashauri na serikali kuu kushirikiana na ushirika katika kuongeza ufanisi kwenye zao la tumbaku kwani natambua
halmashauri zote zinznufaika na tumbaku kupitia ushuru.”alisema.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa aliagiza na kutoa ushauri kwaWETCU,kuhakikisha wataalamu washauri wanakuwa karibu na wakulima ilikutoa huduma za matengenezo ya matrekta hayo,vipuli kupatikana hapahapa Tabora na baadaye huduma hizi zisogezwe hadi wilayani.
Awali katika risala yake,mwenyekiti wa WETCU Alcard Iragila,alisema matrekta hayo ambayo yanakopeshwa kwa vyama vya ushirika
16,yamenunuliwa kwa dola za kimarekeni sh milioni,1,230,000 sawa na sh za Tanzania bilioni 1.8,ikiwa ni sehemu ya mkopo toka benki ya CRDB tawi la Tabora wa dola, 8.74.211 sawa na sh bilioni 12.8 fedha za kitanzania
Aliongeza kuwa kila trekta moja limegharimu dola sh 36,569.56 sawa na sh za kitanzania milioni 53
Iragila alivitaja vyama 16 vya ushirika vinavyokopeshwa matrekta hayokuwa ni Usindi trekta 1,Chapajembe 1,Wema 1,Kigodi 1,Juhudi 1,Limbula1,Amani 1,Mtazamo 1,Itundu 3,Katuma 1 vyama hivyo vyote toka wilaya yaUrambo.
Aidha mwenyekiti huyo alivitaja vyama vingine vya ushirika kuwa chamacha Ugunda toka wilaya ya Sikonge trekta moja na chama cha Itindo tokawilaya ya Uyui trekta 1.

No comments:

Post a Comment