Rais Jakaya Kikwete akiongea na Mwandishi mkongwe, Fili Karashani, ambaye ameshinda tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Tasnia ya Habari mwaka 2011, katika tuzo za (EJAT), zilizoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na washirika wake. Hafla iliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku. Kushoto ni mwandishi wa siku nyingi Khamis Ben Kiko.
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Nevil Meena cheti cha ushindi wa jumla katika tuzo hizo mara baada ya kutangazwa rasmi jana usiku.
Kikundi cha ngoma za asili cha Simba Theatre, kikitumbuiza katika hafla ya utoaji tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda akikabidhi tuzo kwa mwandishi wa habari wa Mlimani Radio, Tuma Dandi mshindi wa habari za watu wenye ulemavu upande wa Radio
Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda, akikabidhi tuzo kwa Abdallah Majura Mkurugenzi wa Radio Sports FM ya Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Brewaries, Graham Andrews, mmoja ya wadhamini wa tuzo hizo, akimkabidhi tuzo, cheti na zawadi yake, Nevil Meena kutoka gazeti la Mwananchi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Executive Solution Agrey Maleale, akimkabidhi zawadi yake Khamis Hamad kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo, baada ya kuibuka mpigapicha bora kwenye tuzo hizo.
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga akizungumza katika hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi walipokutana katika hafla hiyo.
Baadhi ya Watu maarufu waliokuwepo kwenye tuzo hizo, wakibadilishana mawazo.
Baadhi ya majaji walishughulikia tuzo hizo, kutoka kulia ni Itillio Tagalile, Afisa Uhusiano wa Tanesco Badra Masoud na Wenceslaus Mushi wakijadili jambo.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka Mashirika na Makampuni mbalimbali, wakiwa katika hafla hiyo jana usiku.
Baadhi ya Majaji wa tuzo hizo wakiwa katika meza yao, wakibadilishana mawazo.
Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Katibu mtendaji wa Baraza la Habari MCT Kajubi Mukajanga.
Mhariri wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Jaquiline Liana, akizungumza na Mkurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo, Juma Pinto katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Clement Mshana (kulia), akizungumza na Mkurugenzi wa Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Helmans Mwansoko.
Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo, akiwa na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Mkamia.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Teddy Mapunda, akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Fedha wa Kampuni ya hiyo, Graham Anderws.
Bendi ya Msondo ikitumbuiza katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment