TANGAZO


Wednesday, March 21, 2012

Rais Kikwete awaapisha Wakuu wapya wa Mikoa mipya Ikulu


Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akimwapisha Aseri Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, katika hafla ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa mipya minne, Ikulu Dar es Salaam leo.

Mkuu mpya wa Mkoa wa Geita, Magalula Magalula (kulia), akitia saini kwenye fomu ya kiapo baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete (kushoto), Ikulu Dar es Salaam kushika wadhifa huo.

Mkuu mpya wa Mkoa wa Katavi, Rajab Rutenge akiapa kwa ajili ya kushika wadhifa huo Ikulu, Dar es Salaam leo
.

Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa na Wakuu wapya wa Mikoa mipya minne baada ya kuwaapisha Ikulu, Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Rajab Rutenge (Katavi), Magalula Magalula (Geita), Pascal Mabiti (Simiyu) na Aseri Msangi (Njombe).
 
 
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Pascal Mabiti wakifurahia jambo wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wapya wa Mikoa mipya minne leo jijini Dar es Salaam.

Wakuu wapya wa Mikoa, wakipatiwa maelekezo kabla ya kuapishwa, Ikulu, Dar es Salaa leo.

Mkuu wa mpya wa Mkoa mpya wa Njombe, Aseri Msangi.

Mkuu mpya wa Mkoa mpya wa Geita Magalula Magalula.
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Rajab Rutenge.

Mkuu wa mpya wa Mkoa mpya wa Simiyu, Pascal Mabiti
 

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasalimia Wakuu wapya wa Mikoa minne.

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na Makamu wa Rais, Dk. Bilal na Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Wakuu wapya wa Mikoa mipya, baada ya kuwaapisha leo Ikulu jijini.
 

Waandishi wa habari, wakimhoji Mkuu wa Mkoa mpya wa Simiyu, Pascal Mabiti, Ikulu Dar es Salaam leo mara baada ya kuapishwa.

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na ndugu za Mkuu wa Mkoa mpya wa Katavi, Rajab Rutenge, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 

Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa mpya wa Katavi, Rajabu Rutenge na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo, Ikulu Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment