TANGAZO


Wednesday, March 21, 2012

Mbunge Zungu azindua kisima cha maji Shule ya Uhuru Wasichana

 Wanafuzni wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana, wakiwa wamekaa kwenye viwanja vya shule hiyo kwa ajili ya kumsubiri Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', kwa ajili ya hafla ya kukizindua kisima kirefu cha maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali shuleni hapo, leo asubuhi, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Baadhi ya wanafunzi wa madarasa ya awali (chekechea) na msingi wakiwa katika viwanja hivyo leo, wakimsubiri Mbunge wao kwa ajili ya kukizindua kisima kilichojengwa kwa ufadhili wa taasisi ya Africa Muslim Agency kwa gharama ya shs. milioni 7.8


 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Uhuru Wasichana, wakiwa katika hafla hiyo.



 Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akivishwa skafu na chipukizi, Rehema Kondo wakati alipowasili shuleni hapo kwa ajili ya uzinduzi wa kisima hicho.


 Baadhi ya wanafunzi wa madarasa mbalimbali wakiimba wimbo wa kumkaribisha mgeni wakati wa hafla hiyo.



 Chekechea wa shule hiyo, nao wakiimba wimbo huo wa kumkaribisha mgeni, Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' wakati wa hafla hiyo.


 Baadhi ya wanafunzi hao, wakiimba wimbo wa shule hiyo, wakati walipokuwa wakimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa kisima hicho, Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' leo asubuhi.


 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Uhuru Wasichana, Elizabeth Chuma, akizungumza katika hafla hiyo.




 Mwanafunzi Nazimini Abdulkadir, akisoma risala ya wanafunzi wakati wa hafla hiyo.


 Afisa Elimu wa Manispaa ya Ilala, Tatu Kikwete, akizungumza katika hafla hiyo. Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akifuatiwa na Mkurugenzi Mkazi wa taasisi ya Africa Muslim Agency, Bentaleb Mohammed na Mkurugenzi wa Miradi wa taasisi hiyo, Hamisi Bichuka.


 Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kisima hicho, kilichochimbwa kwa ufadhili wa taasisi hiyo. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elizabeth Chuma, Afisa Elimu Manispaa ya Ilala, Tatu Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa taasisi hiyo, Bentalib Mohammed.


 Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kisima hicho, shuleni hapo leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.


 Baadhi ya walimu wa Shule hiyo, wakifuatialia shughuli mbalimbali zilizokuwa zikifanyika katika hafla hiyo.


 Mkurugenzi Mkazi wa taasisi ya African Muslim Agency, Bentalib Mohammed. akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.


 Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, wapiga makofi kwa kufurahisha na majibu mazurin waliyoyapata kutoka kwa bunge wao, 'Mussa Azzan 'Zungu' , wakati akijibu rasala yao katika uzinduzi huo.


 Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akiongoza wageni mbalimbali kwenda kwenye uzinduzi wa kisima hicho.


 Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Africa Muslim
Agency, Bentaleb Mohammed, wakikata utepe ili kukizindua kisima kirefu cha maji ya matumizi
mbalimbali kilichochimbwa kwa ufadhili wa taasisi hiyo, chenye thamani ya sh. milioni 7
kwa ajili ya Shule ya Uhuru Wasichana, huku wakishuhudiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,
Elizabeth Chuma (wa pili kulia) na Afisa Elimu wa Manispaa ya Ilala, Tatu Kikwete, Dar es Salaam leo.



 Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elizabeth Chuma, akimpongeza Mkurugenzi Mkazi wa taasisi ya Africa Muslim Agency kwa ufadhili wa uchimbaji wa kisima hicho, mara baada ya kuzinduliwa na Mbunge Mussa Azzan 'Zungu pamoja na Mkurugenzi huyo. Kulia ni Afisa Elimu wa Manispaa ya Ilala, Tatu Kikwete.


 Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Africa Muslim
Agency, Bentaleb Mohammed, wakikinga maji kutoka kwenye kisima walichokizindua, kilichochimbwa kwa ufadhili wa  taasisi hiyo, chenye thamani ya sh. milioni 7.8 kwa ajili ya Shule ya Uhuru Wasichana, huku wakishuhudiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Elizabeth Chuma (wa pili kulia) na Afisa Elimu wa Manispaa ya Ilala, Tatu Kikwete, Dar es Salaam leo.



 Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Africa Muslim
Agency, Bentaleb Mohammed, wakiwatwisha ndoo za maji, wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru
Wasichana, Belinda Chuwa (kushoto) na Nazimini Abdulkadir wa darasa la saba, mara baada ya
kukizindua kisima kirefu cha maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali, kilichochimbwa kwa ufadhili
wa taasisi hiyo na kugharimu sh. milioni 7.8 kwa ajili ya shule hiyo, Dar es Salaam leo.


 Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, Mkurugenzi Mkazi wa Africa Muslim Agency, Bentaleb Mohammed, Afisa Elimu wa Manispaa ya Ilala, Tatu Kikwete, wakiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Uhuru Wasichana wakikagua eneo la shule hiyo, wakati walipofika shuleni hapo kuzindua kisima kirefu cha maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya shule hiyo, kilichochimbwa kwa ufadhili wa taasisi hiyo.



Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Africa Muslim
Agency, Bentaleb Mohammed, wakiagana baada ya kukizindua kisima hicho katika Shule ya Msingi Uhuru Wasichana jijini Dar es Salaam leo.


Wanafunzi wa shule hiyo, wakikinga maji kwenye chupa baada ya kuzinduliwa kisima hicho na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', jijini leo.

No comments:

Post a Comment