Mkuu wa Wilaya ya Liwale,
Victor Paul Chiwile (pichani) amefariki ghafla jana katika Hoteli ya Vision
mjini Lindi. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila amesema leo kuwa mwili
wa marehemu Chiwile utapelekwa katika Kanisa la Anglikana Lindi ili wananchi
wapate wasaa wa kumuaga kabla ya kusafirishwa kesho kwenda kwao Kibaha kwa
mazishi. Sababu za kifo chake mpaka sasa bado hakijajulikana.
No comments:
Post a Comment