TANGAZO


Saturday, March 17, 2012

Mama Kikwete, azindua matembezi ya mkakati wa Uboreshaji miundombinu ya Elimu Kipawa

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, akiongea na wananchi wa  Kata ya Kipawa, Manispaa ya Ilala, Mkoa wa  Dar es Salaam, Machi 17,2012, wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Uboreshaji wa Miundo-mbinu ya Elimu ya Kata hiyo, ambapo mgeni rasmi alikuwa  Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).



 Baadhi ya wanafunzi wakijipanga kwa ajili ya kuanza matembezi ya Uzinduzi wa Mkakati wa Uboreshaji wa Miundo- Mbinu ya Elimu katika Kata ya Kipawa, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam leo.



 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete (alievaa traki suti ya Blue), akizindua Matembezi ya  Mkakati wa Uboreshaji wa Miundo-mbinu ya Elimu katika Kata ya Kipawa, Manispaa ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam Machi,17,2012. Pichani kutoka kulia wa pili mwenye miwani ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, akifuatiwa na Diwani wa Kata ya Kipawa Bona Kalua, Sherehe hio pia imehudhuriwa na viongozi mbalimballi wa Serikali na wadau wa sekta ya uboreshaji wa miundo-mbinu  ya Elimu na mazingira wa kata hiyo.


 Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete, akikata kitambaa ili kuzindua  Matembezi ya  Mkakati wa Uboreshaji wa Miundo-mbinu ya Elimu katikakata ya Kipawa, Dar es Salaam leo.


Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete, akiongoza matembezi ya uzinduzi wa Mkakati wa Uboreshaji wa Miundo-mbinu ya Elimu katika Kata ya Kipawa, Manispaa ya Ilala, mkoani Dar es Salaam

 Bendi ya Magereza, ikiongoza matembezi hayo.


 Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (mwenye traki suti ya blue) akiongoza matembezi ya Uzinduzi wa Mkakati wa Uboreshaji wa Muindo-mbinu ya Elimu katika  Kata ya Kipawa, Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam. Katika matembezi hayo zilipatikana fedha na ahadi zaidi ya shilingi 18 milioni, ambapo Taasisi ya WAMA wamechangia milioni mbili (2m/-), na Waziri wa Nishati na Madini pamoja na wadau wake wamechangia shilingi milioni10.


 Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akiongoza matembezi hayo.


 Mama Salma Kikwete, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.


 Mama Salma Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Elimu wakati wa uzinduzi wa mkakati huo.


 Mama Kikwete, akisalimiana na Mbunge wa zamani Jimbo la Ilala, mama Martha Wejja, wakati wa uzinduzi wz mkakati wa uboreshaji miundo mbinu ya Elimu leo,


 Baadhi ya wageni na wadau wa Elimu wakiwa wamekaa, wakimsikiliza mama Salma Kikwete, wakati alipokuwa akizunguza katika hafla ya uzinduzi huo.



 Baadhi ya wananfunzi wa Shule ya Kipawa wakiwa wamekaa pamoja na bango lao katika hafla ya uzinduzi huo,


Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea mchango wa shilingi elfu tano kutoka kwa mwanafunzi alieguswa na mkakati wa Uboreshaji wa Miundo- mbinu ya Elimu katika kata ya Kipawa ,Manispaa ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, Machi 17,2012 jijini Dar es Salaam. (kulia) Ni Mstahiki Meya wa  Manispaa ya Ilala Jerry Slaa, akifuatiwa na Diwani wa  Kata ya Kipawa Bona Kalua, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO),

No comments:

Post a Comment