Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko huo tangu ulipoanzishwa 2001. Kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoti na Michael Mhando ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti na Takwimu wa mfuko huo. (Picha na Ricahrd Mwaikenda)
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba, akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Jopo la viongozi wa mfuko huo wakiwa katika mkutano wa kupanga maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa Mfuko.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Celina Wilson, akitaka ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa mfuko wakati wa mkutano huo, leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment