TANGAZO


Friday, March 16, 2012

Maadhimisho Wiki ya Maji yazinduliwa mjini Iringa


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Christina Ishengoma, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), wakati alipotembelea katika banda la Kampuni hiyo katika uzinduzi wa Wiki ya Maji inayofanyika uwanja wa Samora mkoani humo, kuanzia leo Machi 16, ambapo imeelezwa kuwa yatafungwa na Rais Jakaya Kikwete Machi 22. Kampuni hiyo, ndiyo inayodhamini maonesho hayo,  yenye kauli mbiu ya "Maji kwa Usalama wa Chakula". Katikati ni Meneja Udhamini, Nandi Miwyombela. (Picha na Mpigapicha wetu)


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christina Ishengoma, akihutubia wakati wakazi wa  Iringa katika ufunguzi wa maadhimisho hayo.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christina Ishengoma, akipatiwa maelezo na Hamdar Chanzi, Mkemia Mwandamizi wa maabara ya maji Iringa. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maji vijijini Wizara ya Maji na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi maadhimisho ya Wiki ya Maji, Amani Mafuru.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christina Ishengoma, akikata utepe kuzindua rasmi maonyesho ya Wiki ya Maji kwenye Uwanja wa Samora, mkoani humo leo. Kushoto ni Amani Mafuru,  Kaimu Mkurugenzi wa maji vijijini Wizara ya maji.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa,  Dk. Christina Ishengoma, akisikiliza taarifa ya maadhimisho ya Wiki ya Maji kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa maji vijijini Wizara ya maji Mafuru Kaimu, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya maji kwenye Uwanja wa Samora, mkoani Iringa leo.



Kutoka kulia ni Timbe Mkuu wa mahusiano kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Imani Lwinga kutoka (SBL) na Nandi Mwiyombela kutoka (SBL)


Maadamano yakiingia katika uwanja wa Samora mjini Iringa.

Wananchi mbalimbali wakiingia kwa maandam,ano katika uwanja wa Samora.


Kundi la burudani ya Tarumbeya likiongoza maandamano hayo.

No comments:

Post a Comment