Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu safari yake ya kikazi nchini Marekani pamoja na mambo mbalimbali ya kufanikisha maendeleo ya kiuchumi na kidemokrasia nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Hamis Hassan na Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Salum Bimani. (Picha na Kassim Mbarouk)
Baadhi ya wanachama wa Chama hicho, wakisikiliza mazungumzao ya Mwenyekiti wao, Profesa Lipumba kwa waandishi wa habari Ofisi Kuu ya Chama hicho, jijini leo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakifuatilia mazungu ya Profesa Lipumba katika mkutano huo.
Waandishi wa habari, kutoka kushoto, Abubakar Liyongo wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio Ujerumani, George Maziku wa Dira ya Mtanzania na Muhibu Said wa Nipashe wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mwandishi wa habari, Bakari Kimwanga wa Mtanzania, akiwa ameshika kichwa, akitafakari mazungumzo ya Profesa Lipumba, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Ofisi Kuu ya Chama hicho, Buguruni Dar es Salaam leo.
Wapigapicha wa Televisheni mbalimbali wakiwa kazini kurekodi mazungumzo ya Profesa Lipumba kwa waandishi kuhusu safari yake ya kikazi nchini Marekani.
Wanachama wa Chama cha CUF, wakiwa kwenye chumba cha mikutano, wakimsikiliza Profesa Lipumba wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu safari yake ya kikazi, aliyoifanya nchini Marekani.
Baadhi ya wanachama wakiwa nje ya jengo la Makao Makuu ya Chama hicho, wakati wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment