TANGAZO


Sunday, March 18, 2012

Jumuiya ya Wananchi wa Uganda waishio Tanzania Yapata viongozi wake

 Wanajumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, wakiimba wimbo wao wa Taifa, kwenye Ubalozi wao nchini Tanzania, wakati wa Mkutano wao Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wapya, watakaoiongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka 5 ijayo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Msaidizi wa Balozi wa Uganda nchini, Allan Tazenya, akizungumza kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye mkutano huo, wa uchaguzi leo jijini Dar es Salaam.


 Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Ibrahim Mukiibi, akizungumza na wanajumuiya hao kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Jumuiya hiyo leo jijini Dar es Salaam.


 Mwenyekiti wa Jumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, aliyemaliza muda wake, George Kanuma, akizungumza kwenye mkutano huo, kuelezea mambo mbalimbali yaliyofanikishwa na uongozi wake uliomaliza muda wake.


 Mmoja wa wanajumuiya ya wananchi wa Uganda, anayeishi nchini Tanzania, Kiddu Emmanuel, ambaye alikuwa mmoja miongoni mwa walioteuliwa kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo iliyokuwa ikiwaniwa na wanajumuiya watatu, akizungumza kwenye mkutano huo na kuelezea kujitoa kwake kuwania nafasi hiyo na badala yake kumwachia nafasi hiyo, Justus Baguma 'JB', ambaye hatimaye alishinda nafasi hiyo na kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo.


 Mwenyekiti mpya wa Jumuiya wa wananchi wa Uganda, waishio Tanzania, Justus Baguma 'JB', akiwa amekaa pamoja na wanajumuiya wenzake kabla ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, leo Machi 18, 2012, jijini Dar es Salaam.


 Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Ibrahim Mukiibi, akifuatilia kwa karibu uchaguzi huo, ulivyokuwa ukienda. Kushoto ni Katibu wa Ubalozi huo, Dorothy Kalema.


 Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, Justus Baguma 'JB', akipongezwa na Kiddu Emmanuel, aliyejitoa kumpisha (kushoto) na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, George Kanuma.


 Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, Justus Baguma 'JB', akipongezwa na wanajuiya wenzake mara baada ya kumchaguwa kushika nafasi hiyo leo mchana ubalozini hapo


  Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, Justus Baguma 'JB', akipongezwa na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Ibrahim Mukiibi, mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo na wanajumuiya wenzake ubalozini Oyesterbay, jijini Dar es Salaam.


 Mwanajumuiya ya watu wa Uganda , Abantu Baitwababo, akizungumza kutoa maoni yake katika mkutano huo, wa uchaguzi wa viongozi wa wanajumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania.


 Aliyechaguliwa kushika nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Hellen Tusiime, akiwapa mkono Balozi Ibrahim Mukiibi (kushoto) na Mwenyekiti wake, Justus Baguma, mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo kwenye mkutano huo.


 Mgombea wa nafasi ya Ukatibu Mkuu wa wanajumuiya ya watu wa Uganda, waishia Tanzania, Dorothy Kalema, akijieleza kabla ya kupigiwa kura ili kuthibitishwa kwa nafasi hiyo ya uongozi.


 Mwenyekiti mpya wa wanajumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, Justus Baguma 'JB', akizungumza na wanajumiya hao katika kutoa shukurani zake kwa kumchagua kushika nafasi hiyo. Kushoto ni Balozi wa Uganda nchini Tanzania Ibrahim Mukiibi.


 Aliyechaguliwa kushika nafasi ya bwanafedha wa Jumuiya hiyo, Alex Mwijuka, akijieleza kwenye mkutano huo kabla ya kupigiwa kura kwa ajili ya kushika nafasi hiyo.


 Mwenyekiti mpya wa wanajumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, Justus Baguma 'JB', akizungumza na wanajumiya hao kwa ajili ya kufunga mkutano huo, mara baada ya kukamilika kuchaguliwa kwa viongozi wote, watakaoingoza Jumuiya hiyo kwa kipinda cha miaka 5. Kushoto ni Balozi wa Uganda nchini Tanzania Ibrahim Mukiibi.


 Mwenyekiti mpya wa wanajumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, Justus Baguma 'JB', akizunguma jambo na Makamu Mwenyekiti wake Hellen Tusiime, mara baada ya kuufunga mkutano huo.


 Mwenyekiti mpya wa wanajumuiya ya wananchi wa Uganda waishio Tanzania, Justus Baguma 'JB',
akizungumza na Katibu Mkuu wake, mara baada ya kumalizika uchaguzi wa viongozi wapya wa Jumuiya hiyo na kufungwa rasmi kwa mkutano huo na Mwenyekiti huyo.

No comments:

Post a Comment