TANGAZO


Tuesday, March 27, 2012

Hotspot Magazine latoa Ofa za punguzo la bei za bidhaa na huduma

 Mkurugenzi Mkuu wa Hotspot Magazine, Ackland Mhina, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu promosheni ya punguzo la bei za mahitaji mbalimbali kupitia jarida hilo, ambapo mteja akinunua jarida la Hotspot Magazine, linalopatikana kwenye mtandao (website), hutumiwa ujumbe wa kumhakikishia unafuu wa bei kwa huduma atakazozipata ama bidhaa atakazonunua kutoka Makampuni ya New Maisha Club, Khana Khazana Restaurants, Air Uganda, Yami Yami Garden Restaurant, Coco Beach, Samaki Samaki, Afripoa Graphic and Advertising na East African Dream Resort. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari, wakifuatilia mazungumzo hayo, Idara ya habari, Maelezo Dar es Salaam leo.


 Mkurugenzi Mkuu wa Hotspot Magazine, Ackland Mhina, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Ndege la Air Uganda, ambao ni miongoni wa wadhamini wa jarida hilo, Charima Kakuru na katikati ni Mhariri Mkuu wa Hotspot, John Simon.



 Mhariri Mkuu wa Hotspot, John Simon, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kwenye  mkutano huo. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika Shirika la Ndege la Air Uganda, ambao ni moja ya Makampuni wadhamini wa Hotspot Magazine, Charima Kakuru na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa jarida hilo, Ackland Mhina.


Baadhi ya waandishi wa habari, wakifuatilia maelezo, wakati Mkurugenzi Mkuu wa Hotspot Magazine, Ackland Mhina, akizungumza nao kwenye mkutano huo.

2 comments:

  1. ur blog is really nice and interesting, You have maintain it so beautifully that I truly like & enjoy it
    2000 Isuzu Hombre AC Compressor

    ReplyDelete
  2. Thanks alot for your comment. I promise you to give more an excitment news, photos and entertainment events that occurs in Tanzania and other countries

    ReplyDelete