Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara ya nchi za nje kutoka Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya watu wa China, Xiao LU, akizungumza na wadau wa Biashara kutoka China na Tanzania, Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano wa kutangaza maonesho makubwa ya Bidhaa kutoka nchini China ya mwaka 2012, yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China jijini Dar es salaam. Maonyesho hayo yatafanyika mwezi Julai katika viwanja vya maonyesho vya kimataifa vya Dar es Salaam. (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO).
Wadau wa Biashara kutoka China na Tanzania, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakiendela, wakati wa mkutano wa kutangaza maonesho makubwa ya mwaka 2012 ya bidhaa kutoka nchini China yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China jijini Dar es Salaam. (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)
Lin Zhiyong kutoka China akisalimiana na Rais wa Chama Cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda Tanzania (TCCIA), Aloys Mwamanga mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kutangaza maonesho makubwa ya Bidhaa kutoka nchini China ya mwaka 2012 yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment