TANGAZO


Saturday, March 24, 2012

Bonanza la Waandishi wa habari (Media Day), lafana Msasani Beach Club

 Mwandishi wa Gazeti la Jambo Leo, akipiga daluga, huku mwenzake wa Gazeti la Uhuru, akijikinga, ili kuepukana na madhara wakati timu hizo zilipokutana katika mchezo wa mpira wa miguu katika tamasha la Waandishi wa habari (Media Day), lililodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwenye fukwe za Msasani Beach Club, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Mhariri Kiongozi wa Gazeti la michezo la Champion, Saleh Ally, akipiga mpira ili kumalizia pigo la pointi katika mchezo wa wavu (Volly ball), walipokutana na Businass Times, kwenye bonanza hilo.


 Baadhi ya waandishi wa habari, walioingia katika shindano la kucheza ngoma za Ngwasuma, wakishindana kuzirudi ngoma hizo kwenye bonanza hilo.


 Waandishi wa habari wakifuatilia shindano la vijana hao.



 Waandishi kutoka kushoto, Carren Cyprian (IPP), Elizabeth Ndanzi na Dina Ismail wote wa Gazeti la Tanzania Daima, wakiwa katika bonanza hilo.


 Mwandishi mwenye vituko, Iche Mang'enya, akizirudi ngoma za kundi la Ngwasuma sambamba na wanenguaji wa kundi hilo.


 Wanenguaji wa kundi la Ngwasuma, waliokuwa wakitumbuiza katika bonanza la Waandishi wa habari 'Media Day', wakizirudi ngoma kwa ustadi mkubwa na hivyo kutoa burudani safi kwa wanahabari katika bonanza lao hilo, lililodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Msasani Beach Club.


 Mnenguaji wa kundi la Ngwasuma Aisha Juma 'Lokole', akionesha ufundi wake wa kuzirudi ngoma za kundi hilo kwenye bonanza hilo.


 Kundi zima la Vijana waimbaji na wanenguaji wa Ngwasuma wakiwa kazini, kuonesha ustadi wao wa kucheza ngoma za kundi hilo.


 Waandishi nao hawakuwa nyuma walijitosa kwenye ukumbi ilipokuwa ikipiga bendi hiyo na kuanza kuonesha utundu wao katika fani hiyo, kama anavyoonekana mwandhishi Halima Mlacha wa Gazeti la Habari Leo (kulia), akizirudi ngoma pamoja na patna wake.


 Hawa nao, hawakurudi nyuma walijitosa na kuonesha jinsi wimbo wa kundi hilo, unavyoeleza juu ya samaki na vipande vyake.


 Na hawa nao mdadi uliwapanda na kuanza kuingia kichwa kichwa na kufanya vitu vyao katika kuzisakata ngoma za Ngwasuma, iliyokuwa chini ya Kiongozi wake Mkuu, Nyoshi El Saadat.


 Waandishi wa habari, wakijipatia chakula safi kilichotayarishwa maalum kwa ajili yao kwenye bonanza hilo, lililodhaminiwa na TBL na kuendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), fukweni hapo.


 Hawa walikuwa ni baadhi ya wasanii wa makundi mbalimbali yaliyotumbuiza kwenye bonanza hilo.


 Vijana wa ngoma za Wanaume Halisi, wakitayarisha ngoma zao kwa ajili ya kuwaburudisha waandishi kwenye bonanza lao hilo.


 Msanii Bibi Cheka akitumbuiza na kundi lake hilo.


 Kijana, dogo Asley, akitumbuiza na kundi lake hilo kwa wimbo wake maarufu wa 'Naenda kumwambia mama'  na kusababishwa kukatizwa kwa ngoma zake kutokana na waandishi wengi kumvamia na kutaka kupiga naye picha na wengine kucheza naye.


 Mfanyakazi wa East Africa Television (EATV), msanii Masawe Mtata, akipokea zawadi yake ya fedha taslim, kutoka kwa Waziri wa Afrika ya Mashariki, Samwel Sitta, baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika kuzirudi ngoma za Ngwasuma.


 
 Baadhi ya waandishi wa Gazeti la Jambo Leo, wakiwa wamejichanganya na wenzao wa magazeti mengine, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye bonanza hilo.


 Mwandishi wa Radio Uhuru, Cecy, akionesha fedha alizojishindia baada ya kuwa mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake katika kuzirudi ngoma za Ngwasuma.


 Waandishi wa Redio Tumaini, wakiwa kwenye sehemu yao waliyotengewa kwenye bonanza hilo.


 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Blogu hii, Kassim Mbarouk (kushoto), akiwa na wadau wa blogu hii ya bayana kwenye bonanza hilo. (Picha na Mdau Wetu)



 Watangazaji wa Radio Uhuru, kutoka kushoto, Angle Akilimali, Zuhura Zidadu na Emmanuel Barnabas, nao hawakuwa nyuma. Hapa wakiwa kwenye nafasi yao, wakibadilisha mawazo na kufuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka kwenye bonanza hilo.


 Washindi wa kwanza katika mchezo wa Netball, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wakifurahia kombe lao baada ya kukabidhiwa na Mgeni rasmi, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samwel Sitta.


 Wafanyakazi na waandishi wa habari wa Gazeti na Mwana Halisi, wakifurahia kombe lao, waliloshinda katika mchezo wa mpira wa miguu.


 Hawa ni waandishi wa Magazeti ya Business Times, wakisherehekea kombe lao walilokabidhiwa na Waziri Sitta baada ya kuibuka washindi wa jumla katika bonanza hilo.


Mgeni rasmi katika bonanza la waandishi wa habari (Media Day), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samwel Sitta, akizungumza katika bonanza hilo leo, Msasani Beach Club, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo.


 Waandishi wa habari, wakiwa kazini kunasa hotuba na picha ya mgeni rasmi kwenye bonanza hilo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samwel Sitta.


Mgeni rasmi katika bonanza la waandishi wa habari (Media Day), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samwel Sitta, akipunga mkono ili kuwaaga waandishi, wakati akiondoka kwenye bonanza hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo.

No comments:

Post a Comment