Shirika la habari la serikali nchini Senegal limetangaza kuwa rais Abdoulaye Wade amekubali kushindwa na mpinzani wake Macky Sall katika dura ya pili ya uchaguzi wa Urais.
Bwana Wade alimpigia simu mpizani wake Macky Sall, na kumuambia kuwa amekubali kushindwa.
Na maelfu ya wafuasi wa Macky Sall wamejitokeza katika barabara za mji wa Dakar wakisherehekea ushindi wa kiongozi wao.
Miongoni mwa waliokuwa wakisherehekea ni Bi Seynabou Seck
" Niimefurahi sana , Macky bado ni kijana na tena ni mtu mpole sana na ana heshima! Kwa hakika anastahili ushindi huu . Kila mtu alikuwa akimuombea ashinde”.
Mshindi huyo wa duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa urais ameutaja ushindi wake kama muamko mpya kwa raia wa Senegal.
Macky Sall alikuwa akizungumza mara tu baada ya mpinzani wake Abdoulaye Wade mwenye umri wa 85 kukubali kuwa ameshindwa katika duru hiyo ya pili.
Wade alikuwa anataka kuchaguliwa tena kama raia wa Senegal kwa muhula mwengine wa tatu baada ya kubadilisha katiba ya nchi hiyo.
Mabadiliko hayo yalizua machafuko na vurugu kubwa nchini Senegal.
Machafuko hayo halishtua ulimwengu kwani tofauti na jirani zake Senegali imekuwa tulivu na hajawahi kuwa na mapinduzi ya kijeshi kama jirani zake.
Lakini upinzani ulipinga hatua ya kiongozi wao mkongwe na kwenda mahakamani. Hata hivyo mahakama iliidhinisha hatua ya Wade ya kubadili katiba ili aweze kusimama tena kama rais.
Na baada ya dura ya kwanza kukosa kuwa na mshindi wa moja kwa moja kwani hakuna aliyepata zaidi ya asilimia 50, ikiwa ni lazima kuwe na duru ya pili ambapo viongozi wote wa upinzani walimuunga mkoni Macky Sall.
Na sasa Macky Sall ambaye zamani alikuwa Waziri mkuu katika serikali ya Abdoulaye wade ameibuka mshindi.
No comments:
Post a Comment