TANGAZO


Saturday, February 4, 2012

Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Pwani

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akitembelea na kukagua jengo la Shirika la Elimu Kibaha, wakati akimalizia ziara yake ya
Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani leo Februari 04, 2012. Kushoto ni Dk. Isaack Lwali (wa pili
kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu Kibaha, Dk. Cyprian Mpemba. (Picha na
Muhidin Sufiani-OMR)

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikagua jengo la Taasisi ya Utafiti wa maradhi ya Malaria, baada ya kuzindua jengo hilo wakati akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, jana Februari 03, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
 

Makamu wa Rais,   Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dk. Isaack Lwali (wa pili kulia) wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Shirika la Elimu Kibaha, wakati akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani leo, Februari 04, 2012. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu Kibaha, Dk. Cyprian Mpemba.
 
 
 
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua ndani ya jengo la Shirika la Elimu Kibaha, wakati wa ziara yake ya Wialaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani leo.
 
 
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, (katikati), akikata utepe, ili kuzindua Kituo cha Taasisi ya Utafiti wa maradhi ya Malaria kilichopo Bagamoyo, wakati alipokuwa katika ziara yake ya Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani jana Februari 03, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)

No comments:

Post a Comment