Mawaziri wa Ulinzi wa Tanzania, Hussein Mwinyi (kulia), akizungumza na mwenzake wa Msumbiji, Filipe Nyusi, wakati wa hafla hiyo, Ikulu Dar es Salaam leo asubuhi.
Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini, Lindwe Sisulu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Makamu wake, Mohamed Gharib Bilal, katika hafla hiyo, Ikulu leo asubuhi.
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi pamoja na viongozi na wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto), akiwa pamoja na baadhi ya Maofisa wa jeshi katika hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal (nyuma), wakiwa pamoja na Mawaziri wa Ulinzi wa Tanzania na Afrika Kusini, wakifuatilia hotuba ya waziri wa Ulinzi wa Msumbiji (hayupo pichani) katika hafla hiyo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi (katikati), akitia saini makubaliano hayo, huku akishuhudiwa na Rais Jakaya Kikwete (nyuma) na Makamu wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal. Kushoto ni Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Filipe Nyusi na Lindwe Sisulu (kulia) wa Afrika Kusini.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi, akitia saini makubaliano hayo
Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini, Lindwe Sisulu, akitia saini makubaliano hayo.
Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Filipe Nyusi, akitia saini makubaliano hayo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi na Waziri Lindwe Sisulu wa Afrika Kusini, wakibadilishana mikataba hiyo huku wakikumbatiana, baada ya kuisaini leo asubuhi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi (kulia) na mwenzake wa Msumbiji, Filipe Nyusi, wakibadilishana mikataba hiyo, baada ya kuisaini, Ikulu Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Filipe Nyusi na mwenzake, Lindwe Sisulu wa Afrika Kusini, wakibadilishana mikataba hiyo, baada ya kuisaini katika hafla hiyo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza katika hafla hiyo, Ikulu Dar es Salaam leo asubuhi, Februari 7, 2012.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Makamu wake, Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Filipe Nyusi (kushoto), Hussein Mwinyi (kulia) wa Tanzania na Lindwe Sisulu (wa pili kulia) wa Afrika Kusini katika picha ya pamoja mara baada ya kutia saini makubaliano hayo katika hafla hiyo, Ikulu leo asubuhi.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Makamu wake, Mohamed Gharib Bilal (wa pili kushoto), akizungumza na Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini, Lindwe Sisulu (kushoto), mara baada ya kukamilika utaiji saini makubaliano hayo, Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Makamu wake, Mohamed Gharib Bilal (katikati), akibadilishana mawazo na Mawaziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Filipe Nyusi (kushoto), Hussein Mwinyi wa Tanzania na Lindwe Sisulu wa Afrika Kusini, mara baada ya kutia saini makubaliano hayo katika hafla hiyo, Ikulu jijini leo asubuhi.
Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Filipe Nyusi (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kumalizika utiaji saini wa mkataba huo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment