Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo, akitoa maelezo ya awali, kuhusu maendeleo ya kazi za maadalizi ya sensa ya watu na makazi iliyopangwa kufanyika nchini, wakati wa semina kati ya wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati ya Fedha na Uchumi, iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma. Hata hivyo Waziri Mkulo amefafanua kuwa Serikali itahakikisha kuwa sensa hiyo, inafanyika kama ilivyopangwa kwa ubora na ufanisi ikilinganishwa na sensa zilizopita. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO)
Manaibu Waziri wa Fedha Gregory Theu (kushoto) na Pereira Silima, wakifuatilia masuala mbalimbali kuhusu Sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu, wakati semina iliyowahusisha wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati ya Fedha na Uchumi leo Februari 6, 2012, mjini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati ya Fedha na Uchumi wakifuatilia taarifa mbalimbali kuhusu maandalizi ya sense ya watu na makazi, itakayofanyika mwakani, walipokutana na wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo, mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Sensa, Dk. Albina Chuwa, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati ya Fedha na Uchumi, kuhusu zoezi la sensa ya watu, litakalofanyika nchi nzima mwezi, Agosti mwaka huu leo mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment