Ripoti ya Shirika la waandishi wa habari wanaochunguza taarifa, lenye makao mjini London, inaonesha kuwa mamia ya raia wameuwawa katika mashambulio yaliyofanywa na ndege za Marekani zisokuwa na rubani kwenye maeneo ya Pakistan, katika miaka mitatu iliyopita.
Na katika visa vengine, wanavijiji waliokwenda kusaidia kwenye uokozi, waliuliwa katika shambulio la pili.
Rais Obama hivi karibuni alikanusha kuwa raia wengi wamekufa katika mashambulio ya ndege hizo.
Na mashambulio ya ndege zisokuwa na rubani ni swala la mvutano kati ya Marekani na Pakistan.
No comments:
Post a Comment