
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania
(THA), Ephraim Mgawe (kulia) akimkabidhi Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha
Tanzania (TAFFA), Stephen Ngatunga hati ya makubaliano ya kusaidia kupunguza
msongamano wa makontena katika bandari ya Dar es Salaam kwa kuyahamishia katika
Bandari Kavu. Hafla hiyo ilifanyika eneo la Bandari hiyo leo, ambapo taasisi
nyingine nne zilipata hati hizo. (Picha na Richard Mwaikenda)

Naibu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Patrick Kisaka (kushoto) akipokea hati
hiyo, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA), Ephraim Mgawe (kulia) katika hafla hiyo.

Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Tanzania Road
Haulage (1980) LTD, Ali Hussein Lilan akipokea hati hiyo kutoka kwa Mgawe.
Katibu Mkuu wa Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA),
Peter Kirigini (kushoto), akipokea hati kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA), Ephraim Mgawe (kulia) katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment