TANGAZO


Thursday, February 2, 2012

Jaji Mkuu alonga na waandishi kuhusu maadhimisho ya Siku ya Sheria kesho

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Sheria, inayoadhimishwa kesho, nchini kote.  (Picha na Kassim Mbarouk)



Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, akifafanua jambo katika mkutano huo, leo asubuhi, akielezea masuala mbalimbali, ikiwemo ratiba ya maadhimisho, aliyosema yataanza saa 3 za asubuhi, pia alitoa ufafanuzi wa Sheria mbalimbali za nchi baada ya kutakiwa na waandishi kufanya hivyo kwa zile sheria ambazo zimekuwa zikileta mkanganyiko kwa jamii. Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Francis Mutungi. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, wakinakili na kusikiliza ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Jaji Mkuu, Othman Chande, jijini leo asubuhi, Ofisi za Mahakama ya Rufaa.


 Mmoja wa waandishi, wanaoandika habari za Mahakama, kutoka gazeti la Mwananchi, Jame Magai, akitaka ufafanuzi wa moja ya sheria hizo zinazoleta mkanganyiko kwa jamii.


 Msajili wa Mahaka ya Rufaa, Francis Mutungi, akimpatia maelezo mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Happiness Katabazi, wakati wa mkutano huo, kabla ya Jaji Mkuu hajazungumza nao.


 Msajili wa Mahaka ya Rufaa, Francis Mutungi, akitoa ufafanuzi zaidi kwa waandishi hao, kabla ya Jaji Mkuu, Othman Chande kuzungumza nao leo.



Msajili wa Mahaka ya Rufaa, Francis Mutungi, akimsikiliza Katabazi, moja ya masuali yake aliyokuwa akitaka kupatiwa ufafanuzi kutoka kwake.

No comments:

Post a Comment