TANGAZO


Thursday, January 26, 2012

Waziri Mponda awataka madaktari waliogoma kurudi kazini

 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hajji Mponda, akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akiwataka madaktari waliogoma kurudi kazini, ambapo alisema kuwa yupo tayari kukaa nao kwa majadiliano ya madai yao mengine ambayo hayajatekelezwa. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wake, Dk. Lucy Nkya. (Picha na Kassim Mbarouk)



 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya, akifafanua jambo katika mkutano huo, uliowataka madaktari waliogoma kurudi kazini huku wakitakiwa na Waziri Mponda (kushoto), kukaa pamoja kwa majadiliano ya madai yao mengine kwa ajili ya kuyapatia ufumbuzi.



 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hajji Mponda, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo, wizarani hapo leo mchana. Kulia ni Naibu Waziri wake, Dk. Lucy Nkya.

No comments:

Post a Comment