Kompany
Chama cha soka cha England FA kimetupilia mbali rufaa ya Manchester City ya kupinga kadi nyekundu aliyopewa nahodha wake Vincent Kompany, katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Manchester United.
Kompany atakosa mchezo wa kwanza wa nusu fainali wa Kombe la Carling dhidi ya Liverpool na wa marudiano Januari 25.
Pia atakosa mchezo wa ligi dhidi ya Wigan siku ya Jumatatu na dhidi ya Tottenham Januari 22.Katika taarifa yake, FA imesema: "Adhabu hii inajumuisha kukosa mechi tatu kwa rafu mbaya pamoja na mechi mja ya ziada kwa kuwa hii ni kadi ya pili nyekundu msimu huu."
Uamuzi huu utaongeza ghadhabu kwa meneja wa City Roberto Mancini ambaye alitaka wachezaji zaidi baada ya kushangaza wengi siku ya Ijumaa alipodai kuwa klabu hiyo itatetereka katika wachezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya United.
Man City ilitumia takriban pauni milioni 250 kununua wachezaji wapya tangi Mancini alipotajwa kuwa meneja wa klabu hiyo miaka miwili iliyopita.
Hata hivyo klabu hiyo sasa iko mashakani kutokana na kuongezeka kwa majeruhi, huku wachezaji wengine wakiwa wamekwenda kuchezea timu zao za taifa.
Mancini alilazimika kumchezesha Abdul Razak na Denis Suarez kama wachezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya United, na sasa anafikiria kumchezesha beki kutoka Uholanzi mwenye umri wa miaka 17 Karim Rekik.
"Kila mtu anafikiri tuna wachezaji wengi," amesema Mancini. "Lakini tuna wachezaji 19, pamoja na makipa. Sio kikosi kikubwa.
No comments:
Post a Comment