Wananchi wa Arumeru kwa kushirikiana na vijana wa
UVCCM, Taifa wakiufukia mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru mashariki,
Jeremia Sumari wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani
Arusha Leo. (Picha na Haki Ngowi)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa
Arumeru Mashariki, Jeremia Sumari baada ya mazishi yaliyofanyika kijijini
kwao Akheri, mkoani Arusha Leo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa
mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini
kwao Akheri, Mkoani Arusha. Nyuma ni Spika wa Bunge, Anne Makinda na Spika
mtaafu wa Bunge Pius Msekwa.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akitoa heshima zake
za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremia Sumari
kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha Leo.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremia Sumari baada ya mazishi yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha Leo. (Picha na Owen Daudi)
Spika wa Bunge, Anne Makinda akimfariji mke wa Marehemu Mweshimiwa Jeremia Sumari, Miriam Sumari kabla ya mazishi ya marehumu sumari kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha Leo. (Picha na Owen Daudi)
No comments:
Post a Comment