TANGAZO


Monday, January 23, 2012

Makamu wa Rais, Dk. Bilal na miradi ya maendeleo Lindi

 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi jengo jipya la Bwalo la Shule ya Sekondari ya wasichana Ilulu, iliyopo Kilwa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.


 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Kituo cha Afya cha Kitomanga, Lindi Vijijini wakati zaiara yake, mkoani humo jana.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la Msingi, alipozindua Daraja la Mingumbi, Kilwa katika ziara yake hiyo, mkoani Lindi jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Ludovic Mwananzila.



 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea maeneo ya Shule ya Sekondari ya Ilulu, wakati alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuzindua Jengo jipya la Bwalo la Shule ya Sekondari ya wasichana, iliyopo Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoani Lindi jana.



 Makamu wa Rais,  Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Ilulu, baada ya kuzindua rasmi Jengo lao la Bwalo katika ziara yake hiyo jana, Januari 22, 2012.



 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Chumo Namkamba, wakati katika ziara yake hiyo.



Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi katika Ofisi mpya ya Chama cha Mapinduzi CCM, iliyopo Chumo, Namkamba, Kilwa jana januari 22, 2012, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoani Lindi.

No comments:

Post a Comment