|
Rais Mteule wa Cahama cha Madaktari Tanzania (MAT),Primus Saidia akionesha vitabu vya Serikali vinavyoelezea haki za wafanyakazi wa Taasisi za Serikali wakiwemo madaktari, jana wakati wa mkutano mkuu wa madaktari nchini, Dar es Salaam leo , ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu tamko lao la kuitaka Serikali kuwarejesha Hospitai ya Taifa ya Muhimbili, madakari wenzao walioko mafunzoni ambao wamehamishiwa hospitali za kawaida baada ya kuitisha mgomo wa kudai malipo yao. |
|
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Nkopi, akifafanua jambo wakati wa Mkutano wao Mkuu uliofanyika, Dar es Salaam leo, ambapo pamoja na mambo mengine, walirejea tamko lao la kuitaka Serikali kuwarejesha Hospitai ya Taifa ya Muhimbili, Madakari wenzao, walioko mafunzoni, waliohamishiwa Hospitali za Mikoa na nyinginezo baada ya kugoma wakidai malipo yao. (Picha na Richard Mwaikenda) |
|
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Nkopi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo. |
Baadhi ya madaktari waliohudhuria mkutano huo, wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wao katika pia kudai maslahi zaidi.
Baadhi ya wanachama na madaktari waliokuwa katika mkutano huo, wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa kwenye mkutano huo.
No comments:
Post a Comment