TANGAZO


Tuesday, January 24, 2012

Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi

 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi, akizungumza na wadau wa mazingira kutoka Taasisi mbalimbali,wizara na wadau kutoka nchi wahisani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau hao, unaojadili mabadiliko ya Tabia nchi na mkakati wa Kitaifa kuhusu mabadiliko hayo leo jijini Dar es salaam. (Picha na Aron Msigwa)


Mshauri wa masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DFID), nchini Tanzania, Magdalena Banasiak, akizungumzia kuhusu athari za mabadiliko ya Tabia nchi duniani na mchango wa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi  katika kuhakikisha kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi zilizoanza kujitokeza zinadhibitiwa.


 Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi, akiwasilisha mada kuhusiana na mabadiliko ya Tabia nchi na ripoti ya tafiti ya athari za kimazingira iliyofanyika katika baadhi ya maeneo nchini, yakiwemo ya Zanzibar, Mbeya, Tanga, Manyara, Shinyanga na Mwanza leo, jijini Dar es salaam.

 Baadhi ya wadau wa Mazingira kutoka ndani na nje nchi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu mkakati wa Kitaifa unaohusu mabadiliko ya Tabia nchi.

Wadau wa Mazingira kutoka Taasisi mbalimbali, wizara na wadau wa mazingira kutoka nchi wahisani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano unaojadili mkakati wa Kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO)
 











No comments:

Post a Comment