TANGAZO


Tuesday, January 10, 2012

Mbunge Vicky Kamata akabidhi baiskeli kwa wenye ulemavu

 
Mwenyekiti wa Victoria Foundation, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vicky Kamata, akifurahi pamoja na mwananchi mwenye ulemavu kutoka Jimboni lake la Geita baada ya kumkabidhi moja ya baiskeli 30 alizozitoa kwa ajili ya wananchi hao. Msaada huo ni moja ya juhudi za mbunge Kamata katika kunyanyua hali za maisha kwa wananchi wake. (Picha na John Bukuku wa Full Shangwe)
Mbunge Vick Kamata, akizungumza jambo na mmoja wa wazee hao wa Geita.
Mbunge Vicky Kamata, akisukuma baiskeli ya mwanachi mwenye ulemavu, mara baada ya kumkabidhi jana.
Baadhi ya wananchi wenye ulemavu, wakiwa kwenye baiskeli zao, walizokabidhiwa na Mbunge wao, Vicky Kamata (hayupo pichani), Wilayani humo.
Mbunge Kamata, akifurahia jambo na mmoja wa wananchi hao katika hafla hiyo.
Mbunge Vicky Kamata, akizungumza na wananchi katika hafla ya kukabidhi baiskeli hizo.
Baadhi ya wananchi wenye ulemavu, wakisubiri kukabidhiwa baiskeli na mbunge Vicky Kamata katika hafla hiyo.
Baadhi ya baiskeli zilizokabidhiwa kwa wananchi walemavu wa Jimbo la Geita.

No comments:

Post a Comment