TANGAZO


Thursday, January 26, 2012

Airtel yasidia vitabu Shule nne Kilimanjaro

 Wanafunzi na walimu wa shule za sekondari Oshara, Magadini,Kilingi pamoja na shule ya sekondari ya Namwai,zilizoko Wilaya ya Siha,Mkoani Kilimanjaro wakiwa katika halfa ya kukabithiwa vitabu vya kiada zilivyotolewa na kampuni ya simu ya Airtel chini ya mpango wake wa
shule yetu katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shule ya sekondari Oshara jana.


Afisa Uhusiano wa Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel, Jane Matinde, akikabidhi  vitabu kwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Rashid Kitambulo, kwa niaba ya shule nne zilizokabidhiwa vitabu hivyo, vyenye thamani ya sh. milioni 1,  kwa kila shule. Shule hizo ni  Oshara, Magadini, Kilingi pamoja na shule ya Sekondari ya Namwai, zilizoko wilayani Siha, Mkoa wa Kilimanjaro. Kulia ni Mkuu wa shule ya Sekondari ya Oshara, Elieta Kaaya pamoja na Meneja Mauzo wa Airtel, Pascal Bikomagu katika hafla iliyofanyika shule ya Sekondari ya Oshara jana.

 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Oshara, Elieta Kaaya na wanafunzi Reina Kileo na Joseph Mwita, wakipokea vitabu toka kwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Rashid Kitambulo, vilivyotolewa na Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel, chini
ya mpango wake wa shule yetu. Katikati ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde.


 Mkurugenzi  Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid Kitambulo akizungumza na kuishukuru kampuni ya Airtel kwa msaadamkubwa  wa vitabu ilioutoa kwa  shule nne za sekondari zailizopo wilayani hapo,  mwisho kushoto ni  Mwalimu mkuu wa sekondari ya Oshara Elieta Kaaya akifatiwa na wawakilishi wa Airtel Pascal Bikomagu  na Jane matinde (kulia) ni Afisa Elimu Taaluma wa sekondari Wilaya ya Siha,Bw. Mussa Shaban Ally.hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika shule ya sekondari Oshara jana.


Mkurugenzi  Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid Kitambulo(kulia)  akimkabithi vitabu kwa  Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Namwai  Humphrey Kirumbuyo(mwenye suti)  na wanafunzi Felister Mwanga na Hamidu Yusuph Lule msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu, Akishuhudia makabithiano hayo ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde. hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika shule ya sekondari Oshara jana.

No comments:

Post a Comment