TANGAZO


Wednesday, February 8, 2017

Wabunge wapiga kura ya kumchagua rais Somalia

Wabunge wakipiga kura katika eneo la kuwekea ndege ndani ya uwanja wa ndege wa MogadishuHaki miliki ya pichaAMISOM
Image captionWabunge wakipiga kura katika eneo la kuwekea ndege ndani ya uwanja wa ndege wa Mogadishu
Wabunge nchini Somalia wameanza kupiga kura kumchagua rais wa taifa hilo katika uwanja wa ndege ambapo usalama umeimarishwa mjini Mogadishu kwa kuwa maeneo mengine ya mji huo sio salama.
Milolongo ya magari imepigwa marufuku na shule kufungwa huku ndege zikipigwa marufuku kuingia ama hata kutoka mjini Mogadishu ili kuzuia shambulio lolote.
Licha ya hayo yote wapiganaji wa al-Shabab walirusha makombora karibu na eneo la uchaguzi huo usiku wa Jumanne.
Taifa la Somalia linalokabiliwa na vita vya kikabila pamoja na vile vya ukoo halijafanikiwa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia unaoshirikisha raia kushiriki katika uchaguzi tangu 1969.
Uchaguzi huo ulifuatiliwa na mapinduzi ,uongozi wa kiimla na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoshirikisha koo na wapiganaji wa al-Shabab.
Uchaguzi huo unaonekana kama mojawapo ya harakati za kujenga tena demokrasia mbali na kuweka uthabiti.
Usalama umeimarishwa katika maeneo mbali mbali ya mji wa MogadishuHaki miliki ya pichaAMISOM
Image captionUsalama umeimarishwa katika maeneo mbali mbali ya mji wa Mogadishu
Zaidi ya wanajeshi 20,000 wa Umoja wa Afrika wako nchini Somalia ili kuzuia kundi la wapiganaji wa al-Shabab kuipindua serikali dhaifu ya taifa hilo.
Takriban wagombea 20 wanawania wadhfa huo wa urais , huku watatu kati yao wakitarajiwa kusonga mbele kwa raundi ya pili ya upigaji kura ambapo wagombea watakaokuwa wa kwanza na wa pili wataingia katika raundi ya tatu ya kura ya mwisho.
Eneo na uwanja huo linalopigiwa kura ni eneo la kuwekea ndege na limejaa wabunge kulingana na mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi aliyeko huko.
Rais Hassan Sheikh Mohammud anatetea wadhfa wake na wachanganuzi wanasema kuwa huenda akawa miongoni mwa wagombea watakaofuzu katika raundi ya pili na ya tatu.
Uwanja huo wa ndege unaonekana kuwa eneo pekee lenye usalama mkubwa na uchaguzi huo unafanyika hapo baada ya kuondolewa katika taasisi ya mafunzo ya polisi kutokana na wasiwasi wa kiusalama.
Ramani ya taifa la Somalia
Image captionRamani ya taifa la Somalia
Siku ya Jumanne jioni, watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabab walitekeleza msusuru wa mashambulio huku makombora yakirushwa karibu na eneo la uchaguzi huo.
Wakaazi katika kijiji cha Arbacow nje ya Mogadishu wanasema wapiganaji wa Jihad walishambulia kambi ya Umoja wa Afrika katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment