TANGAZO


Tuesday, December 6, 2016

Sergio Aguero: Nyota wa Manchester City kukosa mechi nne

Sergio Aguero akimkabili David LuizImage copyrightREX FEATURES
Image captionManchester City walilazwa 3-1 nyumbani na Chelsea Jumamosi
Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amepigwa marufuku kucheza mechi nne baada yake kufukuzwa uwanjani kwa uchezaji mbaya mara ya pili msimu huu.
Aguero, 28, alifukuzwa uwanjani kwa kumchezea visivyo beki wa Chelsea David Luiz wakati wa mechi ambayo City walilazwa 3-1 nyumbani Ligi ya Premia siku ya Jumamosi.
Mshambuliaji huyo wa Argentina alikuwa ameadhibiwa tena mwezi Agosti alipopewa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo mchezaji wa West Ham Winston Reid.
Atakosa mechi za City dhidi ya Leicester, Watford, Arsenal na Hull.
Mwenzake wa City Fernandinho pia alifukuzwa uwanjani alipokabiliana na Cesc Fabregas baada ya madhambi hayo ya Aguero na amepigwa marufuku kucheza mechi tatu.
Wachezaji wengine wa City walikabiliana.
Fernandinho amsukuma FabregasImage copyrightREX FEATURES
Image captionFernandinho anamsukuma Fabregas ambaye anaonekana kumzaba kofi
Fernandinho amsukumaFabregasImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionFernandinho anaonekana kukasirika na kumkaba kooni Fabregas na kumsukuma nyuma
Fabregas anaangukaImage copyrightREX FEATURES
Image captionMaafisa wa Chelsea wanaingilia kati, Fernandinho mara nyingine tena anamsukuma Fabregas, ambaye anaangukia mabango ya matangazo

No comments:

Post a Comment