Maafisa wa usalama wa Somalia wanasema makao makuu ya polisi mjini Mogadishu, yameshambuliwa.
Watu 13 wameuawa wakiwemo raia 5.
EPA
Kulikuwa na milipuko mikubwa na moshi mwingi, baada ya washambuliaji waliojitolea mhanga, kwenye magari mawili yaliyosheheni mabomu, walipovurumisha magari kwenye mlango wa idara ya upelelezi wa uhalifu.
Inasemekana wapiganaji tena walivamia jengo.
Siku chache zilizopita, watu 13 waliuwawa kwenye mashambulio mawili ya magari yaliyokuwa na mabomu, mjini Mogadishu pia - shambulio lilofanywa na wanamgambo wa kiislamu kutoka Somalia al-Shabab.
EPA
Kundi la wanamgambo la al-shabab linadai kuwa ndilo lilitekeleza shambulizi hilo.


No comments:
Post a Comment