Mmoja wa nyota wa mpira wa vikapu duniani Kobe Bryant, amecheza mechi yake ya mwisho ya kulipwa nchini Marekani.
Mchezo huo umefikisha kikomo uchezaji wake wa zaidi ya miongo miwili ambapo Bryant amekuwa wa tatu kwa kuandikisha alama nyingi zaidi katika historia ya mchezo huo.
Alishinda mataji matano ya NBA akiwa na LA Lakers ambao amewachezea muda wote huo.
Kwenye mchezo huo dhidi ya Utah Jazz uwanja wa Staples Center mjini Los Angeles, California Lakers walitoka nyuma na kushinda 101-96.
Bryant alitwaa alama 60, ikiwa ni mara yake ya sita kufanya hivyo katika mechi moja. Anayemshinda kwa hilo ni Wilt Chamberlain pekee.
Getty
Tiketi za mechi hiyo yake ya mwisho, zimekuwa zikiuzwa hadi dola 30,000 za Kimarekani.
Lakini mwandishi mmoja wa BBC anasema Bryant hajaenziwa kwa njia sawa na mashabiki.
Reuters
Wakati mwingine alikuwa hachezaji vyema na mara kwa mara alikorofishana na machezaji mwenzake, Shaquille O'Neal.
Mwaka 2003 alituhumiwa kumbaka mwanamke mmoja lakini baadaye wakaafikiana na kumaliza kesi nje ya mahakama.
Bryant, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 37 alianza kucheza katika ligi ya NBA moja kwa moja baada ya kumaliza shule ya upili akiwa na umri wa miaka 17.
Aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mchanga zaidi kujiunga na NBA, akicheza dhidi ya Dallas akiwa na umri wa miaka 18, miezi miwili na siku 11.


No comments:
Post a Comment