TANGAZO


Thursday, September 4, 2014

Benki ya Azania yazindua Akaunti mpya ya Dhamira Account jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Singili, akizungumza, wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya benki hiyo, ya Dhamira account, Dar es Salaam leo. Kushoto ni waandishi wa habari, waliohudhuria uzinduzi wa akaunti hiyo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Singili, akizungumza, wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya benki hiyo, ya Dhamira account, Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Singili, akimkabidhi fomu ya kujiunga na akaunti mpya ya benki hiyo, ya Dhamira account, wakati wa uzinduzi wa akaunti hiyo, Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Singili, akimuelekeza mteja wa kwanza, Naomi Mapunda, jinsi ya kujaza fumo ya kujiunga na akaunti mpya ya Dhamira, wakati alipokuwa akiizindua akaunti hiyo, Dar es Salaam leo.
Mteja wa kwanza, Naomi Mapunda, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukabidhiwa fomu kujiunga na akaunti hiyo mpya ya Dhamira, wakati wa kuzinduliwa, Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Singili, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya benki hiyo, ya Dhamira account, Dar es Salaam leo.

Magendela Hamisi
WATANZANIA wa pato la chini na kati wanaweza kufikia malengo ya kuondokana na umaskini kwa kujiwekea akiba kidogo kidogo na kutimiza ndoto zao maishani ikiwemo kufungua biashara ambazo zitaweza kutoa ajira vijana wengi nchini.

Hatua hiyo ya mafanikio inaweza kufikia ikiwa wananchi wataweza kujiwekea utaratibu maalumu katika maisha yake ya kawaida hali itatofanya kuwa na nidhamu ya kutunza fedha na baadaye kutumiza dhamira iliyokusudiwa.
Hayo yalibanishwa jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Azania, Charles Ngili wakati akizindua akaunti ya mpya ya dhamira yenye lengo la kuchochea tabia ya watu kujiwekea akiba kwa ajili ya kufanya kitu maalumu kwa kutimiza ndoto anachohitaji maishani mwake.

Akaunti ni nzuri hasa kwa wale wanaohitaji kumiza malengo kama vile kununua kiwanja, kusomesha, kufunga na kuendeleza biashara na kufikia mtaji wa biashara kubwa, kwani mteja atachagua utaratibu na muda maalumu wa kuweka akiba mara kwa mara.
Alifafanua kuwa akaunti hiyo mteja anaweza kuweka akiba kuanzia sh. 50,000 kila mwezi na atalipwa riba ya asilimia 8 isiyokuwa na makato, hali inayotoa fursa kwa wananchi wa rika kuanzia miaka 18 kufungua akaunti hiyo.
Katika uzinduzi wa dhamira akaunti, mteja Naomi Mapunda ambaye ni mjasirimali, alifanikiwa kuwa wa kwanza kufungua akaunti hiyo na kutoa mwito kwa wananchi wengine kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kutimiza malengo yao maishani.


"Nashukuru kuwa wa kwanza kufungua akaunti hii,ninaamini nitapata mafanikio makubwa kwani baada ya kipindi fulani nitaweza kuongeza mtaji wa biashara yangu ambayo itaweza kutoa ajira wa wengine," alisema.

No comments:

Post a Comment