Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Henry Lihaya akimkaribisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara(wa pili kushoto waliokaa0 wakati wa uzinduzi wa ligi ya Dar es Salaam Community Cup leo katika viwanja vya shule ya msingi Turiana Magomeni jijini Dar es Salaam. Ligi hiyo inashirikisha timu 12 kutoka shule za Sekondari za jiji la Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija - Wizara ya Habari)
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na washiriki wa mashindano ya Mpira wa miguu yajulikanayo kwa jina la Dr es Salaam Community Cup leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua rasmi mashindano hayo, kushoto ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na washiriki wa mashindano ya Mpira wa miguu yajulikanayo kwa jina la Dr es Salaam Community Cup leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua rasmi mashindano hayo, kushoto ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na kulia ni Katibu Mtendaji wa TFF Selestine Mwesigwa.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikagua wachezaji wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mpira wa miguu yajulikanayo kwa jina la Dr es Salaam Community Cup leo jijini Dar es Salaam kulia ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akipiga penati kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya Mpira wa miguu yajulikanayo kwa jina la Dr es Salaam Community Cup leo jijini Dar es Salaam , aliyeko gorini ni ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Moja ya timu zinazoshiriki mashindano hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
Moja ya timu zilizopambana katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo, wakiwa katika picha ya pamoja.
Mchezaji wa Shule ya Sekondari Turiani akidhibiti mpira wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Idd Azzan (kushoto) akimpa matibabu mchezaji wa Shule ya Sekondari Kawe Thomas Ibrahim aliyeumia wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Dar es Salaam Community Cup leo katika viwanja vya shule ya msingi Turiani.

No comments:
Post a Comment