TANGAZO


Tuesday, October 15, 2013

Rais Jakaya Kikwete aonana na viongozi wa Vyama vya Upinzani, Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Singida kupitia cha cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu. Nyuma ni James Mbatia NCCR Mageuzi, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, kupitia Chadema, John Mnyika.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mzungumzo na Viongozi wa Vyama vya Siasa vya Upinzani, Ikulu jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara. Phillip Mangula (kulia kwa Rais), leo. 
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkaribisha Ikulu, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, Dar es Salaam leo. Nyuma kushoto ni Kiongozi wa NCCR Mageuzi James Mbatia na Professa Ibrahim Lipumba wa CUF.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya Upinzani muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu muswaada wa rasimu ya Katiba, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Wengine katika picha kutoka kushotoni Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe Chadema, Phillip Mangula CCM na Bibi Nancy Mrikaria, aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP, Agustine Lyatonga Mrema.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya upinzani na wasaidizi wao, waandamizi muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu muswaada wa rasimu ya Katiba Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto mbele Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM na Bibi Nancy Mrikaria, aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP, Agustine Lyatonga Mrema. Waliosimama Nyuma kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu CUF, Julius Mtatiro, Tundu Lissu Chadema, Martin Mng’ong’o, NCCR Mageuzi, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi, Habib Mnyaa wa CUF, Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe. (Picha zote na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment