MENEJA WA SHIRIKA LA POSTA MKOA WA MBEYA HASSAN
MWANG'OMBE AKIZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI (HAWAPO PICHANI) KATIKA HAFLA YA
KUWAPONGEZA WAFANYAKAZI WAO.
WATUMISHI wa Umma na sekta binafsi nchini wameaswa
kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kuleta ufanisi katika kuziletea
manufaa sekta wanazofanyia kazi.
Mwito huo umetolewa na baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika
la Posta Tanzania ambao wametunukiwa Zawadi za wafanyakazi bora kutokana na
utendaji kazi wao baada ya kupigiwa kura na watumishi
wenzao.
Wakizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na
uongozi kwa wafanyakazi wote iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa
uliopo Sokomatola Jijini Mbeya baada ya kupewa nafasi ya kuwashukuru wenzao kwa
kuwawezesha kuchaguliwa wafanyakazi bora wa Mwaka 2013.
Leonard Yegella (Principal Finance Officer-
usimamizi)ambaye pia alitunukiwa zawadi ya mfanyakazi bora na Raisi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete alisema anafurahia kupewa
nafasi kama hiyo ambayo ameipata kutokana na ushirikiano mzuri na wafanya kazi
wenzie.
Wengine waliotunukiwa zawadi na Uongozi wa Posta ni
pamoja na Bi Genoveva G. Assenga karani wa Posta kutoka makao makuu Dar Es
Salaam, Bi. Magreth Mabula na Mkosa Shaban Madanganya walioibuka wafanyakazi bora
kutoka Mkoa wa Mbeya.
|
No comments:
Post a Comment