TANGAZO


Monday, April 30, 2018

SIMBA ILIVYOIPIGA YANGA BAO 1-0 UWANJA WA TAIFA KATIKA MCHEZO WA LIGI KUU YA VODACOM JIJINI DAR ES SALAAM JANA

Mashabiki wa Simba wakiwa kwenye jukwaa lao Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana kushuhudia timu yao, wakati ikipambana na watani wao wa jadi Yanga katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mashabiki wa Yanga wakiwa kwenye jukwaa lao Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana kushuhudia timu yao, wakati ikipambana na watani wao wa jadi Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom. 
Timu za Simba na Yanga zikiongozwa na waamuzi wa mchezo huo, zikiingia uwanjani tayari kuanza mpambano wao huo. 
Kikosi cha Simba kikipiga picha ya pamoja na vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino), katika kampeni ya kuwalinda dhidi ya majanga ya kushambuliwa na madhara mengine.
Kikosi cha Simba kikipiga picha ya pamoja na vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino), katika kampeni ya kuwalinda dhidi ya majanga ya kushambuliwa na madhara mengine. 
Kelvin Yondani wa Yanga akimtoka Shomari Kapombe wa Simba katika mchezo huo. 
Emmanuel Okwi wa Simba akipiga mpira mbele ya beki wa Yanga, kelvin Yondani. 
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akiudhibiti mpira uliokuwa ukifuatiliwa na Ibrahim Ajib wa Yanga.  
Nicholas Gyan wa Simba akijaribu kumpiga chenga Raphael Daudi wa Yanga.
Mchezaji wa Simba, Erasto Nyoni (kulia goli), akiwa amekabwa na PapyTshishimbi, akijitayarisha kuupiga mpira kichwa kilicho zaa bao pekee katika mchezo huo, na kuipa Simba pointi tatu katika mchezo huo.
Wachezaji wa Simba, Erasto Nyoni (katikati), John Bocco (kushoto) na Emmanuel Okwi wakishangilia bao hilo, lililofungwa na Nyoni. 
Nicholas Gyan wa Simba akimtoka Raphael Daudi wa Yanga katika mchezo huo. 
Mashabiki wa Yanga wakiwa wameduwazwa baada ya Simba kufunga bao hilo. 
Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya timu yao kufanikiwa kuilaza Yanga katika mchezo huo. 
Ubao wa Matokeo ukionesha Simba bao 1 na Yanga 0. 
Ubao wa Matokeo ukionesha Simba bao 1 na Yanga 0, baada ya kukamilika dakika 90 za mchezo huo pamoja na za nyongeza.  
Wachezaji wa Simba wakiwa na kocha wao, Pierre Lechantre pamoja na Msaidizi wake, Masoud Djuma, wakishangilia baada ya kumalizika kwa mchezo huo na  kuibuka na ushindi wa bao 1 - 0 dhidi ya watani wao, Yanga. 

No comments:

Post a Comment