Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo dhidi ya Al Masry ya Misri katika mchezo wa kwanza wa Kombo la Shirikisho barani Afrika, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao 2-2.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ubao wa matangazo ukionesha Simba 1 Al Masry 2 mpaka dakika ya 75 ya mchezo huo.
Mchezaji Laudit Mavugo wa Simba akiumiliki mpira huku akifuatwa na Mohamed Koffi wa Al Masry.
Laudit Mavugo wa Simba akizongwa na Mohamed Koffi wa Al Masry.
Mohamed Koffi wa Al Masry akimbana Laudit Mavugo wa Simba.
Ahsante Kwasi wa Simba akiumiliki mpira huku akijaribu kumpiga chenga Islam Atta wa Al Masry.
Ahsante Kwasi wa Simba na Islam Atta wa Al Masry, wakiwania mpira katika mchezo huo.
Ahsante Kwasi wa Simba na Islam Atta wa Al Masry, wakikimbia kila mmoja akiwania kuumiliki mpira katika mchezo huo.
Emmanuel Okwi wa Simba akiumiliki mpira huku akifuatwa na Mohamed Koffi wa Al Masry.
Golikipa wa Al Masri, Ahmed Abdelwahab, akiwa amejirusha bila mafanikio kuwani kuudaka mpira wa penalti uliopigwa na Emmanuel Okwi bila mafanikio, baada ya kutolewa adhabu hiyo kutokana na beki Mohames Koffi wa Al Masri kuunawa mpira ndani ya boksi la 18 na hivyo Okwi kuiandikia timu yake bao la pili na hivyo timu hizo kumaliza mchezo huo kwa kufungana mabao 2-2.
Emmanuel Okwi akiukimbilia mpira ili kuwa kuanza baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha huku golikipa wa timu ya Al Masry, Ahmed Abdelwahab, akiwa bado amekaa chini.
Hapa ubao wa matangazo ukionesha Simba 2 Al Masry 2 mpaka mwisho wa mchezo huo ulisimama baada ya kutokea mvua kubwa na kukatika kwa umeme uwanjani hapo katika dakika ya 80 ya mchezo huo.
Mashabiki wa Simba wakiwa na furaha tele baada ya timu yao kulazimishwa sare baada ya kutangulia kufuga bao la kwanza katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment