TANGAZO


Monday, February 12, 2018

Uwanja wa London wafungwa baada ya bomu la vita vya pili vya dunia kupatikana

London City Airport

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLondon City Airport
Uwanja wa ndege wa mjini London umefungwa baada ya bomu la vita vya pili vya dunia kupatikana kwenye mto ulio karibu wa Thames.
Uwanja huo utafungwa siku nzima na safari zote za ndege kufutwa, na kuwaathiri hadi abiria 16,000.
Bomu hilo liligunduliwa siku ya Jumapili eneo la George V wakati wa shughuli ya kikazi mashariki mwa London.
Uwanja huo ukafungwa na polisi wanasema kuwa wanashirikiana na jeshi la wanamaji kuondia bomu hilo.
Police cordon near London City Airport
Image captionPolisi wakiwa London City Airport
Abiria wameambiwa wasisafiri kwenda uwanja huo na kushauriwa kuwasiliana na mashirika yao ya ndege.
"Uwanja wa ndege unashirikiana kabisa na polisi wa Met na jeshi la wanamaji kuliondoa bomu hilo kwa njia salama na kutatua suala hilo haraka iwezekanavyo," alisema Robert Sinclair, mkurugenzi mkuu wa uwanja huo.
Ndege zinazotumia uwanjai huo wa London City ni pamoja na British Airways, Flybe, CityJet, KLM na Lufthansa kwa safari za ndani na kwenda nchi zingine zaUlaya.
London City AirportHaki miliki ya pichaPA
Image captionUwanja huo utapanuliwa kwa gharama ya pauni milioni 400

No comments:

Post a Comment