Klabu ya Manchester City imekubali mkataba wa kumsajili kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk's 24 na raia wa Brazil Fred kwa dau la £44.5m mwisho wa msimu huu. (Goal)
Klabu za Manchester City na Manchester United zina hamu kumsajili beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire, 24. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 28, analengwa na AC Milan, ambayo iko tayari kutoa dau la £32m kumsajili mchezaji huyo wa Uhispania.(Tuttosport via Express)
Chelsea huenda ikamuajiri mkufunzi wa zamani wa Hull na Watford Marco Silva kusimamia klabu hiyo kwa muda mfupi iwapo watamfuta kazi Antonio Conte kabla ya mwisho wa msimu huu.. (Times - subscription required)
Mshambuliaji wa Ubelgiji 27, Eden Hazard amesema kuwa katika soka lolote linawezekana kabla ya kuongeze kwamba anafurahia kuichezea Chelsea wakati alipoulizwa kuhusu kuhusishwa kwake na Real Madrid. (Marca)
Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 25, hajapinga uhamisho kurudi katika klabu yake ya zamani Real Madrid. Alipoulizwa iwapo anaweza kurudi Real Madrid alisema kuwa anafurahia kusalia na Blues lakini akaongezea kuwa ''Madrid ni Madrid''.(Mail)
Real Madrid wanaamini itakuwa rahisi kumsajili kipa wa Chelsea Thibaut Courtois, 25, mwisho wa msimu huu ikilinganishwa na kipa wa Manchester United David de Gea, 27. (Independent)
Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane ametaja kuwa habari za uongo kuhusu ripoti kwamba klabu hiyo inapanga kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania, 25 Isco. (El Pais - in Spanish)
Arsenal na Chelsea wote wanataka kumuajiri kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique kuwa meneja wake.. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 26, huenda akabaini kwamba kazi yake katika klabu hiyo imekwisha kufuatia kuwasili kwa aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Dortmund-Emerick Aubameyang, 28, kulingana na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Emmanuel Petit. (sun)
No comments:
Post a Comment