Wachezaji wa Azam FC wakiingia uwanjani kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Simba SC, Dar es Salaam leo jioni. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wachezaji wa Simba SC wakiingia uwanjani kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam FC, Dar es Salaam leo jioni.
Benchi la Ufundi la Azam FC.
Kikosi cha Simba SC kilichopambana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kikosi cha Azam FC, kilichopambana na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni na kukubali kichapo cha bao 1-0.
Benchi la Ufundi la Simba SC.
Wachezaji wa Simba SC, wakiwasalimia mashabiki wao kabla ya kuanza mchezo huo, dhidi ya Azam FC.
Mashabiki wa Simba FC wakifuatilia mchezo kati ya timu yao dhidi ya Azam FC.
Emmanuel Okwi wa Simba SC, akimtoka Yakub Mohamed wa Azam FC katika mchezo huo.
Bruce Kangwa wa Azam FC akiudhibiti mpira huku akizongwa na Shiza Kichuya wa Simba SC.
Emmanuel Okwi wa Simba akiwatoka Yakub Mohamed (kulia) na Bruce Kangwa wote wa Azam FC.
Emmanuel Okwi (kushoto) wa Simba akiwania mpira na Bruce Kangwa wa Azam FC.
Wachezaji john Bocco, Emmanuel Okwi (katikati) na Said Ndemla wakishangilia bao pekee katika mchezo huo, lililofungwa na Okwi.
Emmanuel Okwi (kushoto), Nahodha John Bocco na Said Ndemla (kulia), wote wa Simba wakishangilia bao hilo, pekee alililofungia timu yake.
Emmanuel Okwi (wa pili kulia), akishangilia bao hilo, huku akipongezwa na wachezaji wenzake.
Ubao wa matokeo ukionesha Simba SC bao 1 na Azam FC 0.
Wachezaji wa Azam FC wakimzonga na kumlalamikia mwamuzi wa mchezo huo, Jonesia Rukyaa baada ya kupiga filimbi ya adhabu kuelekea langoni kwao katika mchezo huo.
Asante Kwasi (kulia) wa Simba SC, akiwania mpira na wachezaji Daniel Amoah (3) na Ennock Atta wote wa Azam FC.
Dakika ya 47 ya kipindi cha pili Simba SC ikiwa mbele kwa bao 1 na Azam FC 0, kama ubao wa matangazo ulivyokuwa unaonesha.
Mashabiki wa Simba SC wakishangilia ushindi wa timu yao hiyo, kwa kuwasha fataki mara baada ya mwamuzi Jonesia Rukyaa, kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo huo.
No comments:
Post a Comment