Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akikagua moja ya jalada la mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ili kujiridhisha juu ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akimhoji Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba sababu za kutomchukulia hatua mmoja wa watumishi mwenye tatizo la cheti licha ya kuwepo taarifa ambazo zinamuwezesha kuchukua hatua.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika kikao na Maafisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ili kujiridhisha juu ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa Halmashauri hiyo. Afisa Tawala Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Zephania Mshanga (katikati) akipitia orodha ya watumishi waliohakikiwa vyeti vya ufaulu wa kidato cha nne na cha sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika mazungumzo ya kikazi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi, Bw. Clodwing Mtweve alipomtembelea Ofisini kwake Katibu Tawala huyo. Katikati ni Afisa Tawala Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Zephania Mshanga akifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.
No comments:
Post a Comment