TANGAZO


Tuesday, February 6, 2018

MAANDALIZI YA MCHEZO WA NGUMI JUMUIYA YA MADOLA, TIMU YA TAIFA YA NGUMI YASISITIZWA KUHUSU NIDHAMU

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo akizungumza na timu ya taifa ya mchezo wa ngumi kuhusu masuala ya nidhamu alipowatembelea leo kambini katika  uwanja wa ndani wa michezo  jijini Dar es Salaam, ambapo wanajifua kwa ajili ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajia kufanyika nchini Australia mwezi Machi mwaka huu. Wa kwanza kushoto ni Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Bw. Gulam Rashid na wapili ni kushoto ni Katibu Mkuu Shirikisho la  Ngumi  Bw.Makore Mashaga.(Picha zote na Anitha Jonas – WHUSM)
Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Bw. Gulam Rashid akieleza Timu ya Taifa ya Ngumi jitihada zinazofanywa na ofisi yake kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika nchini Australia Machi Mwaka huu leo alipowatembelea kambini katika uwanja wa ndani wa michezo jijini Dar es Salaam,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo.
Mabondia wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Ngumi wakiendelea na mazoezi walipotembelewa leo kambini na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo (hayupo pichani) katika uwanda wa ndani wa michezo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea maandalizi yao kwa mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarijiwa kufanyika nchini Australia Machi mwaka huu kushoto ni Bondia Alex Sita na Mhina Morice (kulia).   
Mabondia wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Ngumi wakiendelea na mazoezi walipotembelewa leo kambini na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo (hayupo pichani) katika uwanda wa ndani wa michezo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea maandalizi yao kwa mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarijiwa kufanyika nchini Australia Machi mwaka huu kushoto ni bondia Mwaite Juma na Saidi Ramadhani (kulia). 
Kapteni wa Timu ya Taifa Mchezo wa Ngumi ya wanaume  inayojiandaa kwa ajili ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika nchini Austaralia Bw.Seleman Kidunda akitoa taarifa ya timu na shukrani huku akisistiza kuwa timu imejiaanda vizuri kwa mashindano kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo (hayupo pichani) leo alipowatembelea kambini katika uwanja wa ndani jijini Dar es Salaam.
Kapteni wa Timu ya Taifa Mchezo wa Ngumi ya wanawake inayojiandaa kwa ajili ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika nchini Austaralia Bi. Zulpha Macho akitoa taarifa ya timu na shukrani huku akisistiza kuwa timu imejiaanda vizuri kwa mashindano kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo (hayupo pichani) leo alipowatembelea kambini katika uwanja wa ndani jijini Dar es Salaam.  
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo (aliyevaa shati la kitenge)akiwa katika picha ya pamoja na timu ya taifa ya mchezo wa ngumi inayojiandaa na mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika nchini Australia Machi Mwaka huu alipowatembelea kambini leo katika uwanja wa ndani wa michezo jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment